Wananchi wa mtaa wa Airtel katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
wameiomba Serikali kuwasaidia kuboresha daraja ambalo limekuwa likijaa maji
katika kipindi cha mvua
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio
na kusema kuwa daraja hilo limesombwa na kujaa maji na kusababisha wananchi
kushindwa kuvuka na wengine kusombwa na maji hayo.
Hivi karibuni
wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA mkoani Katavi imesema kuwa upo mpango wa kukarabati barabara
na madaraja yote ya mijini na vijijini ili kupunguza ubovu wa miundombinu.
Tatizo la miundombinu maeneo mengi mkoani Katavi kipindi
cha masika limekuwa kikwazo kwa wananchi
kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment