Baadhi ya
wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamelazimika kusitisha huduma kutokana na ubovu wa
miundombinu.
Mpanda Radio imefika
katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Mpanda na kuzungumza na baadhi
ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji ambazo zinatumia barabara ya
mpanda-tabora.
Kwa sasa magari
yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo yameamriwa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma
ambapo wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanalazimika kuongeza nauli kwa
shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa
safari umeongezeka
Hata hivyo wamesema
kuwa barabara mbadala ya kupitia uvinza nayo haipo kwenye hali nzuri kitendo
kinachosababisha ugumu wa safari.
Mwishoni mwa wiki
iliyopita mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza
kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji
Chanzo:Haruna juma
No comments:
Post a Comment