Wito umetolewa kwa
watumishi katika sekta mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
mkoani Katavi kujituma katika kazi zao ili wananchi waweze kupata huduma.
Ameyasema hayo
mkurugenzi wa manispa ya Mpanda Michael Nzyungu wakati akizungumza na Mpanda
Redio kwa njia ya simu kuhusu mapungufu ya watumishi katika halmashauri baada
ya sakata la watumishi hewa ambalo limeathiri sekta mbalimbali za kiutendaji
hapa nchini zikiwepo Afya ,elimu,utawala.
Aidha amesema kuwa
swala la watumishi hewa halijaathiri Halmashauri japo kuwa kuna mapungufu ya
kudumu kwa watumishi katika sekta mbalimbali.
Serikali kupitia kwa wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika April 9 mwaka
huu Bungeni imeagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote wa Umma waliofukuzwa
kimakosa ikiwemo wale walioishia darasa la saba.
CHANZO:Rebecca Kija
No comments:
Post a Comment