Baadhi ya
Wafanyabiashara wa Soko la Misufini mtaa
wa Rungwa kata ya kazima mkoani Katavi wamebainisha changamoto wanazokabiliana
nazo baada ya kufanya biashara katika soko hilo kwa takribani miezi miwili
sasa.
Wakizungumza na Mpanda Radio
wafanyabiashara hao wamesema kumekuwa na changomoto mbalimbali ikiwa ni pamoja
na uchafu,miundombinu na baadhi ya wafanyabiashara waliokaidi kuhamia sehemu
elekezi.
Mwenyekiti wa soko hilo
Bi Neema Rashid amesema changanoto hizo wameshazifikiisha kwa wahusika wanacho
subiri ni utekelezaji na kuwaomba wafanyabiashara kufanya kazi kwa ushirikiano
ili kudumisha biashara zao.
Soko la misufini
linajumuisha wafanyabiashara wadogowadogo wanaouza nyanya,mahindi, viazi,
ndizi,mchele, na bidhaa nyinginezo.
CHANZO:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment