Mwenyekiti wa
Kamati ya miundombinu Bungeni ambaye pia
ni Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini
Sulemani Kakoso amewataka wasafiri wanaosafiri kutoka Mpanda kwenda Tabora
kutumia njia ya Treni mpaka barabara itakapotengenezwa.
Ameyasema hayo wakati
akizungumza na Mpanda Radio leo kupitia kipindi cha Kumekucha Tanzania na
kusema kuwa tayari wameshazungumza na meneja wa shirika la Reli ili waweze
kuongeza behewa litakaloweza kupunguza adha ya usafiri.
Insert.kakoso
Aidha Kakoso amesema
serikali imejipanga
kufanya matengenezo ya dharura katika barabara zote nchini ambazo zimeharibiwa
na mvua inayoendelea kunyesha .
Tarehe 14 mkuu wa mkoa
wa Katavi Meja Jenerali Raphael Mhuga aliagiza barabara ya Mpanda –Tabora
kufungwa kutokana na mvua iliyoharibu barabara hiyo
chanzo:Rebecca
kija
No comments:
Post a Comment