Wafanyabiashara wa soko
la Buzogwe katika Halmashauri ya Manipaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba Halmashauri kuweka huduma ya maji na umeme
katika soko hilo ili kunusuru biashara zao.
Akizungumza na Mpanda Radio mwenyekiti wa soko hilo Ramadhani
Athumani amesema kitendo cha kutokuwa na
umeme katika soko hilo kinafanya biashara ziwe hatarini kwani wezi wanaweza
wakaiba kwa urahisi kutokana na usalama kuwa mdogo
Aidha ameiomba
Halmashauri kuliangalia swala hilo kwa haraka kwani walinzi wanatumia tochi
kulinda wakati wa usiku hali ambayo huatarisha mali za wafanyabiashara katika
soko hilo.
Katika hatua nyingine
ameishukuru halimashauri kwa kujenga choo lakini ameiomba kuboresha huduma ya
maji ili madhara ya magonjwa ya mlipuko yasiweze kutokea soko hapo.
chanzo:rebecca
No comments:
Post a Comment