Wakazi
wa kata ya Kapalala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi
wamesema,kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio kimechochea maendeleo kwa kiasi
kikubwa kutokana na kutangaza habari na vipindi vinavyoigusa jamii.
Wakizungumza
na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti wakazi hao wamesema,jamii imekuwa na uelewa
wa mambo mengi yanayolenga katika sekta ya afya,kilimo,elimu,usafiri
pamoja na miundombinu mbalimbali ikiwemo
barabara.
Kwa
upande wake Daud Peter Nyasio ambaye ni mwenyekiti wa kijiji katika kata hiyo
ameishukuru Mpanda Radio kwa jinsi inavyofikisha ujumbe kwa wananchi huku
akisema usikivu mzuri umesaidia wananchi kuelimika kwa kiasi kikubwa.
Kituo
cha kijamii cha Mpanda Radio kinachopatikana eneo la Mtaa wa Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2013.
Chanzo:Isaack
No comments:
Post a Comment