Wakazi wa kijiji cha
Mtakuja kilichopo Kata ya Kapalala wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wameitaka
serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili waondokane
na adha ya ukosefu wa maji safi na salama.
Wengi wanazishutumu
mamlaka kushindwa kuwajika kwa kuchukua hatua za haraka badala yake zimekuwa
zikitolewa ahadi zisizo tekelezeka.
Mwenyekiti wa kijiji hicho
Daud Peter Nyasio amekiri kuwepo kwa kero ya maji katika kijiji hicho na kueleza kuwa
visima viwili vilivyopo haviwezi kutosheleza idadi ya wananchi ambao idadi yao
ni zaidi ya elfu tatu.
Hata hivyo Reward
Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya
Mtakuja,Songambele na Kapalala amesema kuwa hana jambo lolote la kuzungumza kuhusu
suala la maji katika kata ya Kapalala kwani kila wanapoomba pesa serikalini
hazitolewi kama inavyotakiwa.
Chanzo Issack Gerald
No comments:
Post a Comment