Chama cha
ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimefanya maazimio ili kuishinikiza serikali
kuchukua hatua stahiki juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi inayo wakabili wananchi katika maeneo mbali mbali mkoani
Katavi.
Katibu wa
Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi Joseph Mona amewaambina wanahabari kuwa
shabaha ya kikao hicho ilikuwa ni kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya
mkoa inavyo shughurikia kero hizo.
Mara kadhaa
Chama hicho kimetaja waziwazi kuwa kero hizo zimetokana na kutwaliwa na
serikali kwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa kile kinacho
daiwa kuwa ni maeneo yaliyo katika hifadhi za misitu.
Katika
hatua nyingine Mona ameyataja baadhi ya mapendekezo yatakayo wezesha kufikia
hatima ya migogoro hiyo kuwa ni pamoja na Serikali kutumia njia shirikishi
kabla ya kufanya maamuzi sanjari na utekelezaji wake utakao kwenda sambamba
na kuheshimu misingi ya kisheria.
Mwaka 2017
mwezi agost mamia ya wananchi katika vijiji vya Mgorokani, kata ya
Stalike, na Kijiji cha Nsambwe Kata ya
Kanoge waliondolewa kinguvu katika makazi yao kwa madai ya kukaidi maagizo ya
serikali yaliyokuwa yakiwataka kuhama katika vijiji hivyo kwa madai ya kuwa ni
hifadhi za misitu.
Chanzo: Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment