Mamlaka ya kukusanya Mapato
TRA katika Mkoa wa Katavi imeanza zoezi la kuhakiki namba za utambuzi wa kwa wafanyabiashara
zinazojulikana kama Tini Namba
Akizungumza na Mpanda redio
ofisini kwake Meneja wa TRA mkoa Enos Mgimba amesema zaidi ya wafanyabiashara Elfu
nne wanatarajia kufanyiwa uhakiki huo katika mkoa na kwa sasa zoezi hili limeanza
hapa Manispaa na baadae litahamia katika maeneo mengine ya mkoa
Aidha Mgimba amebainisha
kuwa faida ya utambuzi wa tini namba kwa wafanyabiashara huwasaidia wao kama mamlaka
kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara hali ambayo huwasaidia katika kukusanya
mapato pamoja na kuwasaidia wateja wao panapotokea shida mbalimbali za kibiashara
Ametoa wito kwa wafanyabiashara
hao kufika katika ofisi hizo kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki wa Tini namba za biashara
zoezi hilo limeanza leo 18/4/2018 na linatalajia kukamilika tarehe 27/4/2018
Chanzo:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment