Baadhi wananchi wa Mtaa wa Mpanda Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi wamesema Daftari la uandikishaji wa majina kwa wageni limeweza
kupunguza uharifu katika mtaa huo.
Wakizungumza na Mpanda Redio Kwa nyakati tofauti tofauti wamesema mpango wa serikali wa kuanzisha daftari la
majina kwa wageni wanao hamia kutoka sehemu nyingine imekua ni silaha tosha kwa
jamii nzima ya mtaa huo kwani wanapata nafasi ya kumjua kila mgeni anayehamia
katika maeneo hayo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa mtaa
huo Afredy Mtaita amesema kuwa
kuanzishwa kwa daftari hilo kumesababisha
takwimu ya uharifu kupungua kwa kiasi kikubwa tofauti na mwaka jana.
Aidha mwenyekiti huyo amesema
kwamba tayari wameshaunda kamati ya ulinzi shirikishi kwa jamii
itakayoweza kutokomeza uhalifu katika mtaa huo pia amewaomba wananchi wa mtaa
huo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake katika jamii.
No comments:
Post a Comment