Wakulima wa kata ya
Kakese Mbugani Halmashauri ya manspaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba
serikali kuendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazao ya nafaka.
Wameyasema hayo wakati
wakizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa wengi wao hawana elimu hiyo hali
inayosababiisha kuendelea kuhifadhi
mazao hayo kienyeji na kusababisa hasara.
Kwa upande wake
mtendaji wa kata hiyo Felix Kalonga amesema kuwa elimu hutolewa katika mikutano
ya hadhara lakini wananchi wengi wamekuwa hawahudhurii mikutano hiyo.
Kuhifadhi mazao ya
nafaka kupitia elimu itolewayo na
wataalamu wa kilimo huwasaidia wakulima wengi kuepuka na uharibifu wa mazao
hasa yanayokaa kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment