Waislamu mkoani Katavi wameaswa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani
ili kupata rehema ,msamaha na kujiepusha na moto.
Sheikh wa Mkoa wa Katavi Sheikh Ally
Husein akizungumza na Mpanda
Radio amesema waislamu hasa vijana wamekuwa wakikaidi kufunga kwa sababu
mbalimbali.
Sheikh Husein amesema si jambo jema kwa muislamu kuacha kufunga mwezi
mtukufu bila udhuru kwani kufunga ni
amri ya Mwenyezi Mungu.
Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za dini ya
kiislamu.
No comments:
Post a Comment