Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema,hana
taarifa za jeshi la polisi kutoshirikiana na serikali za mitaa katika kata ya
Misunkumilo hasa nyakati za usiku kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama.
Kamanda Nyanda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano na Mpanda Radio
kufuatia taarifa za hivi karibuni kuwa kwa sasa ulinzi shirikishi haufanyiki
katika kata ya Misunkumilo kutokana na ukosefu wa ushirikiano kati ya
polisi,wananchi na viongozi.
Aidha Kamanda Nyanda ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za
viashiria vya uhalifu ili kuudhibiti kabla ya kusababisha madhara.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Misunkumilo Bw.Januari
Kayungilo amekiri kuwepo ulinzi hafifu katika kata hiyo lakini amesema mikakati
inapangwa ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika ulinzi ikiwemo
kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaelimisha wananchi.
Hivi karibuni,Mwenyekiti wa Mtaa wa Misunkumilo Bw.Katabi Jonas alikiri
kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi huku jeshi la polisi
nalo likiwa limejiweka kando kwa sasa.
No comments:
Post a Comment