Afisa uhamiaji wa Mkoa wa
Katavi Vicent Haule amewataka wananchi
kushirikiana na jeshi hilo katika kuwafichua wananchi ambao sio watanzania
maarufu kama wahamiaji haramu .
Ameyasema hayo wakati akizungumza
na Mpanda Radio ofisini kwake nakusema kuwa njia ambazo wanazitumia katika
kuwabaini wahamiaji zimesaidia kupunguza ongezeko la wahamiaji hao .
Aidha Haule ameongeza kwa kutaja
kazi za jeshi hilo na malengo yake ikiwa ni pamoja na kuimarisha mipaka ili
kudhibiti wahamiaji haramu.
Pia amesema kuwa ulinzi na usalama
ni jukumu la kila mwananchi hivyo wanapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya
ulinzi na usalama ili kupata msaada wa haraka.
CHANZO:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment