Wakulima zao la Tumbaku
katika mkoa wa Katavi wameaswa kuacha Tabia ya kuchanganya Tumbaku chafu
maalufu kama Ngulai kwenye msimu huu wa masoko ya zao hilo unaoendelea sehemu
mbali za mkoa kwa wakulima wa zao hilo.
Wito huo umetolewa na
mwakilishi wa Kampuni ya Premiumu Tanzania katika mkoa wa katavi bwana Iddy
Ramadhani wakati akizungumza na mpanda redio kuhusu mwenendo wa masoko yanayo
endelea katika maeneo ya mkoa.
Aidha Ramadhani amesema
katika msimu huu wa kilimo 2017/2018 kampuni hiyo inatalajia kununua zaidi ya
kilo millioni sita za tumbaku kutoka katika vyama vya msingi vya wakulima wa
Tumbaku vilivyopo katika mko wa katavi
Katika siku za hivi
karibuni zao la tumbaku limekuwa likipigwa vita kutokana na changamoto ya
uhalibifu wa mazingira katika kuzalishwa kwake na sasa kunampango maalumu
unaotekelezwa na serikali kwa kuanzisha kilimo cha mazao mengine kama vile
pamba, kolosho na alizeti.
No comments:
Post a Comment