Serikali ya Mkoa
wa Katavi na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT
wamesaini mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Kaimu katibu
tawala Bw.Wilbrod Malandu akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini
kwake,amesema Bodi ya Zabuni imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa
ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76
ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda 76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya
juu.
Aidha Malandu
amesema eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana
Kata ya Kazima ambapo zaidi ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia
watu 108 ili kupisha ujenzi .
Kwa upande wake
Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga
taifa SUMA JKT Kanali Andrew Mkinga pamoja na kuipongeza serikali ya mkoa wa
Katavi kwa kumpatia zabuni hiyo,ameahidi kujenga kwa weledi na kukamilisha kazi
kwa wakati uliopangwa.
Mkoa wa Katavi
ulianza Mpango wa ujenzi wa hospitali ya Rufaa tangu mwaka 2014 ambapo katika
eneo la ujenzi kunatarajia kuwemo vitengo mbalimbali vikiwemo Chuo cha sayansi
na tiba,chuo cha uuguzi na utafiti pamoja na shule,maduka,hotel, stendi ya
mabasi na viwanja vya michezo.
CHANZO:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment