Baraza maalumu la
madiwani katika halmashauri ya wilaya yam panda mkoani katavi wameazimia
kuundwa kwa timu ya uchunguzi ili kuchunguza ujenzi wa maabara katika shule za
sekondari.
Maazimo hayo yamekuja
baada baraza hilo kubaini kuwepo kwa kasoro katika ujenzi wa maabara hizo na
kuwepo kwa ongezeko la gharama tofauti na zilizokuwepo kwenye mikataba ya
awali.
Kwa upande wa mkuu wa
wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameitaka timu hiyo kufanya utekelezaji wa
haraka ili ujenzi huo uweze kukamilika na ameiagiza mamlaka ya Takukuru na
vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi na ikibainika kuna ubadhilifu wa
fedha hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Shule ambazo timu hiyo
itapita kukagua na kujiridhisha na ujenzi majengo ya maabara ni sekondari ya
kalema,ikola,kabungu,mwese,katuma na mpanda ndogo.
CHANZO:Rebecca Kija
No comments:
Post a Comment