Wakulima katika kata ya
kakese halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamelalamikia kudolora
kwa bei ya mazao ya chakula hali ambayo haiwasaidii kujikwamua kutoka Kwenye dimbwi la umaskini.
Wakizungumza na mpanda
Redio wamesema inawalazimu kuuza kiasi kikubwa cha mazao ilikujikimu kuendesha
maisha yao na kupelekea kushidwa kujenga nyumba bora kutokana na bei ghari ya
bidhaa za ujenzi zinavyo uzwa madukani kutokana na bei ndogo ya mazao.
Kwa upande wake diwani
wa kata ya kakese Maganga Salaganda
amesema changamoto hiyo ipo na kuiomba serikali kuandaa utaratibu wa
masoko na kuruhusu mazao kuuzwa nje ya nchi ilikuwa kuwakomboa wakulima.
Mkoa wa Katavi ni miongoni
mwa Mikoa hapa nchini inayo tajwa kwa kuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa
mazao ya chakula kama vile Mpunga mahindi na karanga.
Chanzo:
Paul Mathius
No comments:
Post a Comment