Mkuu wa wilaya ya
Tanganyika Salehe Mhando amewapongeza wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya
maskini Tasaf kwa kuanzisha miradi mbali
mbali ya maendeleo katika kata ya kabungu kwani itasaidia kukua kiuchumi.
Ameyasema hayo wakati
wa ziara ya kukagua miradi hiyo ambayo inatekelezwa na wanufaika wa Tasaf iliyopo
katika kata hiyo ikiwemo shamba la miti
aina ya mitiki na visima vitatu.
Kwa upande wao
wanufaika wa miradi hiyo wamesema kuwa fedha ambazo wamekuwa wakipata
zimewasaidia kuendesha maisha yao na kuendelea kiuchumi.
Katika ziara hiyo mkuu
wa wilaya alitembelea na kukagua miradi ya Tasaf katika kijiji cha
kabungu,mchaka mchaka,vikonge na Igalula.
Mpango
wa kunusuru kaya maskini ni mmoja ya mipango ya kitaifa unaotekelezawa nchini
ukiwa na lengo la kuziwezesha kaya maskini ili kuongeza kipato, fursa na uwezo
wa kugharamia mahitaji muhimu ya kibinaadamu kama vile chakula, afya na elimu.
Chanzo: Restuta
No comments:
Post a Comment