Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo amezindua treni ya kwanza ya abiria katika reli mpya ya kisasa {SGR} iliyojengwa kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Reli hiyo ina urefu wa kilomita 472 ambapo treni zitakuwa zikisafiri kwa kasi ya wastani ya kilomita 120 kwa saa na kutumia muda wa saa nne na nusu kutoka Mombasa hadi kufika Jiji la Nairobi, ikiwa ni safari ambayo ilikuwa ikitumia takriban saa 8 kwa njia ya basi.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia uzinduzi huo wamesema treni hiyo itakuwa mkombozi kwao kwa madai kuwa hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa katika kusafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Rais Kenyata wakati akipokea mfano wa treni ya mizigo itakayosafiri katika reli ya kisasa
No comments:
Post a Comment