Na Mussa Mbeho.
WAJASIRIAMALI wadogo wadogo wanaojishughulisha na
utengenezaji wa fenicha mbalimbali mkoani Tabora wameiomba serikali
kutenga eneo maalumu litakalowasaidia kujenga kiwanda kikubwa ambacho
kitasaidia kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao pamoja na ajira kwa vijana mkoani
humo.
Ombi hilo limetolewa leo na Bwana Francis Beatus na Said
Mrisho wakati wakizungumza na mpanda radio fm mara baada ya
kutembelea katika kiwanda hicho na kujionea jinsi ambavyo vijana hao
wakiendelea na shughuli zao.
Aidha vijana hao wameongeza kuwa mbali na kukabiliwa na
changamoto hiyo ya ukosefu wa eneo lakini pia wanakabiliwa na changamoto
ya upungufu wa vifaa vya kufanyia kazi hali ambayo inapelekea uzalishaji
kungua siku hadi siku na kufanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa
kiwanda hicho Bw. Manyambo Mrua
amesema kiwanda hicho kimekuwa kikitoa ajira na mafunzo ya ufundi
kwa vijana hivyo serikali inapaswa kuwasaidia kwa kutenga eneo ambalo
litawasaidia kujenga kiwanda kikubwa ili kuweza kutoa ajira zaidi kwa
vijana pamoja na kuendeana na sera ya serikali ya uchumi viwanda.
Hata hivyo bwana murua ameiomba
serikali kuwasaidia katika kuboresha vitendea kazi na kuwatengea eneo
litakalo mudu kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.
No comments:
Post a Comment