Wakati ikiwa haijatimia hata wiki moja tangu aliyekuwa nahodha wa Manchester United Wayne Rooney kurejea kwenye klabu yake ya kwanza ya Everton, mchezaji huyo amefunga bao lake la kwanza kwenye ardhi ya Tanzania katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Mtanange huo uliopigwa Alhamis Julai 13, kwenye Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar e Salaam, umehudhuriwa na idadi kubwa ya watazamaji waliojawa na hamu ya kumuona nyota huyo aliyedumu Manchester kwa takribani miaka 13.
Watanzania na hata baadhi ya raia kutoka mataifa mengine ya bara la Afrika, wanacho cha kujivunia zaidi kwa kuwa ndio watu wa kwanza duniani kumshudia nahodha huyu wa England, akishuka dimbani tangu kurejea kwake Everton.
Rooney aliifungia goli la kuongoza klabu yake hiyo kwa shuti kali kutokea karibu kabisa na eneo la katikati ya uwanja na huenda bao hilo limetuma salaamu kwa kocha wake Ronald Koeman, mashabiki na ulimwengu mzima kuwa yeye bado ni imara kabisa katika kuzifumania nyavu.
Hata hivyo goli hilo la Rooney alilofunga dakika ya 34 ya mchezo, halikuweza kudumu kwa muda mrefu, kabla mchezaji Jacques Tuisenge kuisawazishia klabu yake ya Gor Mahia katika dakika ya 36.
Kipindi cha pili Rooney hakurejea dimbani, japo kukosekana kwake hakukuiathiri sana timu yake hiyo, kwani dakika 82, mchezaji Kieran Dowell alipachika bao la pili na la ushindi katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya ushindi wa bao 2-1 kwa Everton.
Mbali na ardhi ya Tanzania kujiwekea rekodi itakayosalia katika vichwa vya wapenda soka duniani, mwamuzi Israel Mkongo naye amejiwekea rekodi ya kuvutia ya kuchezesha mtanange huo uliovuta hisia za watu wengi ndani na nchi ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Mahindi MAHINDI yanaendelea kuwadodea wakulima mkoani Rukwa baada ya wafanyabiashara na watu binafsi kuchangamkia mahindi kut...
No comments:
Post a Comment