Monday, 17 July 2017

MAPACHA WALIOUNGANA WAFAULU KIDATO CHA SITA .

Maria na Consolata waona ulemavu sio mwisho wa kutimiza ndoto zao
Pacha walioungana, Maria na Consolata wamejawa na furaha baada ya kufaulu mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita, katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa, Kusini magharibi mwa Tanzania.

Maria na Consolata, walio na umri wa miaka 19, wamefaulu kwa kupata daraja la pili katika masomo yao ya kidato cha sita na kuwa na matumaini kuwa ndoto yao ya kuwa walimu hapo baadaye inaelekea kutimia. Maria na Consolata wameieleza BBC furaha yao:

"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," ameeleza Consolata. Mabinti hawa wangependa kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Ruaha mkoani humo. Wameeleza sababu za kuchagua chuo kwenye mkoa wanaoishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao wangependa kubadili mazingira.

"Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi. Pia ni kwa sababu kwa hali yetu tulivyo hatumudu kuishi kwenye mazingira ya joto. Mji wa Iringa ni baridi, hali hii tumeizoea.

'' Maria na Consolata wanaona kuwa, hakuna linaloshindikana iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu " Wazazi washukuru Mungu kupata watoto wenye changamoto kama wao wasione kuwa na mtoto mlemavu ni laana.
 Pili wawaone kama watoto wengine na kuwapa mahitaji yao ya msingi, wawawezeshe, wawapatie nafasi ya kujiendeleza maana wakiwezeshwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.''

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...