Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini
Fortonatus upande wa kulia akiwa na kikosi chake wakikagua moja ya mabasi ya abiria jana alfajili katika kituo cha mabasi jijini Mbeya. |
Mbeya.
Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu ameagiza askari saba
wa kikosi hicho katika Kituo Kikuu cha Mabasi Mbeya waondolewe kituoni hapo kwa
madai ya kuruhusu mabasi mabovu kubeba abiria.
Kamanda Musilimu
alimuagiza Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya (RTO) Butusyo Mwambelo
kutekeleza amri hiyo jana baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika mabasi
na madereva eneo hilo.
“Hawafanyi kazi
ipasavyo na hii inatokana na kukaa kituo kimoja zaidi ya miaka mitano,” alisema
Kamanda Musilimu.
Pia, alisitisha
mabasi matano kutoendelea na safari baada ya kubaini hitilafu kwenye mfumo wa
usukani na magurudumu.
Ofisa Mfawidhi wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) Mkoa wa Mbeya,
Denis Daud alisema chombo cha moto lazima kifanyiwe ukaguzi na maofisa wa
polisi kama kina sifa ya kuingia barabarani.
Mdau wa usafiri,
Mohamed Abdalah alisema ukaguzi uliofanywa na kamanda unaisadia kubaini mabasi
ambayo hayaruhusiwi kuwapo barabarani.
@mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment