Raisi Uhuru Kenyatta na naibu wake William Rutorfi |
Kesi ambayo kiongozi
wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga anapinga kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru
Kenyatta, itaanza kusikilizwa rasmi jumapili saa tisa mchana na kuendelea hadi
Tarehe moja mwezi ujao ambapo majaji saba watatoa uamuzi wao.
Kesi hiyo ilianza
jumamosi kwa maelezo ya mwanzo ambayo kila upande ulitoa ili kuhakikisha nafasi
kwa kusikilizwa rasmi.
Katika kikao cha
kwanza ambacho kilichukua muda wa masaa matano, na kumalizika saa tano
usiku,mawakili wa pande zote walitoa maombi yao na matakwa yao ya
kisheria.
Ombi kuu alilotoa
James Orengo, mmoja wa mawakili wa Raila Odinga lilikuwa mahakama kumruhusu
kumulikwa kwa mitambo ya kompyuta ambayo imehifadhi hati rasmi za uchgaguzi
uliofanywa mapema mwezi huu.
Hata hivyo ombi la
Orengo lilipingwa vikali na mawakili wanaomwakilisha rais Uhuru Kenyatta na pia
tume inayosimamia uchaguzi Kenya.
Majaji
wa mahakama hayo ya juu Kenya wanatarajiwa kutoa uamuzi wao saa nane
leo mchana ikiwa watamruhusu ama kukataa ombi la wakili Orengo, kumulika
kompyuta inayohifadhi hati za uchaguzi.
No comments:
Post a Comment