Wafuasi wa Raila Odinga, wakati wa maandamano mbele ya Mahakama Kuu ya Kenya, Nairobi tarehe 18 Agosti 2017 |
Jumatatu hii Agosti 28 asubuhi Majaji saba wa mahakama ya juu nchini Kenya wataanza kusikiliza kesi ambayo kiongozi wa upinzani Raila Odinga anapinga kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, 2017.
Kesi
hiyo ilianza siku ya Jumamosi kwa maelezo ya mwanzo ambayo kila upande ulitoa
ili kuhakikisha nafasi kwa kusikilizwa rasmi.
Katika
kikao cha kwanza ambacho kilichukua muda wa masaa matano, na kumalizika saa
tano usiku,mawakili wa pande zote walitoa maombi yao na matakwa yao
ya kisheria.
Ombi
kuu alilotoa James Orengo, mmoja wa mawakili wa Raila Odinga lilikuwa mahakama
kumruhusu kumulikwa kwa mitambo ya kompyuta ambayo imehifadhi hati rasmi za
uchgaguzi uliofanywa mapema mwezi huu.
Hata
hivyo ombi la Orengo lilipingwa vikali na mawakili wanaomwakilisha rais Uhuru
Kenyatta na pia tume inayosimamia uchaguzi Kenya.
Majaji
wa mahakama hayo ya juu Kenya wanatarajiwa kutoa uamuzi wao saa nane leo mchana
ikiwa watamruhusu ama kukataa ombi la wakili Orengo, kumulika kompyuta
inayohifadhi hati za uchaguzi.
Hayo
yakijri Mahakama ya juu nchini Kenya usiku wa Jumapili kuamkia lJumatatu hii
imekubali kuingizwa kwa ushahidi kwenye kesi ya kupinga matokeo ya urais, hatua
ambayo sasa imetenga uwanja wa makabiliano ya hoja kati ya mawakili wa rais
Uhuru Kenyatta na wale wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Tofauti na ilivyokuwa mwaka 2013, majaji saba wa
mahakama hiyo walitupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na mawakili wa pande
zote mbili waliotaka kila mmoja ushahidi wake utupwe kwa sababu uliwasilishwa
nje ya muda.
No comments:
Post a Comment