McGregor alifanikiwa kwenda hadi katika raundi ya 9 lakini
ilipofika raundi ya 10 mambo yalibadilika baada ya Mayweather kumshambulia sana
hadi Gregor aliyekuwa hoi sana huku ikiwa imebaki dakika 1:55 kwa pambano
kuisha.
Ushindi wa asubuhi ya leo umezidi kumpa rekodi nzuri Mayweather
ambapo sasa Mmarekani huyo anakuwa amecheza mapambano 50 ya mashindano bila
kupigwa.
McGregor alitabiriwa kupigwa kabla hata ya mchezo huu kutokana
na uzoefu wa Mayweather katika mchezo wa boxing na alionekana kuzidiwa kweli
dakika za lala salama za pambano hilo na Mayweather akatumia mwanya huo
kumuangusha.
Katika raundi ya 1 na ya 2 hadi 3 McGregor alionekana alionekana
kummudu Mayweather huku refa akamuonya kutokana na aina ya upigaji wake ambapo
alionekana kumpiga Mayweather chini ya kichwa.
Baada ya raundi ya 4 kuisha na Gregor kuonekana mchangamfu,
kibao kilianza kubadilika raundi ya 5 ambapo alianza kuonekana kuchoka na
ilipofila ya 8 McGregor alionekana hoi zaidi ndipo ya 10 alishambuliwa sana
akiwa hoi bina taaban.
Baada ya mchezo huo Floyd alisema “nimewapa mashabiki kile
walichotaka kukiona, baada ya mpambano ya Pacquao niliwaahidi kwamba nitarudi
kuwafurahisha na leo wameona nilichofanya” alisema Mayweather huku akisisitiza
“ni mpambano wangu wa mwisho.”
No comments:
Post a Comment