Wednesday, 23 August 2017

Meya wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda amewashauri wanaotarajia kubomolewa makaazi yaliyo katika hifadhi ya reli kuondoka kabla ya muda waliopewa kufika.

Meya wa katavi Mh. william Mbogo

MPANDA.
Wakaazi wa mtaa wa msasani na Tambuka reli katika manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambao wanatarajia kubomolewa makaazi yao ifikapo mwezi januari mwakani kwa madai ya kuishi ndani ya hifadhi ya reli wameshauriwa kuondoka kabla ya muda huo kufika ili kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza. 
Ushauri huo umetolewa na Mstaiki Meya wa manispaa ya Mpanda William Mbogo wakati akizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa ni vema kupuuza maneno ya baadhi ya watu wanaowashawishi kutoondoka katika maeneo hayo. 
Meya Mbogo amesema kutokana na hali hiyo tayari wameanza mpango wa kuawaandalia maeneo katika mtaa wa kampuni  ambayo wakaazi hao wanaweza kujenga.

Meya William Mbogo aliomgezea kusema aidha tayari kuna baadhi ya wakaazi wa mtaa wa msasani na tambuka reli ambao wameanza kuhamia katika mtaa wa Kampuni kwa ajili ya kuanza makazi Mapya.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...