Wednesday, 23 August 2017

Wakazi wa kitongoji cha mgolokani kata ya Starike mkoani Katavi wanaishi chini ya miti kutokana na makazi yao kuharibiwa na serikali.

Wakazi wa kitongoji cha mgolokani kilichopo kata ya Starike katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kusini magharibi mwa Tanzania wanaishi chini ya miti tangu zoezi la kuharibu makazi yao lilipo fanywa mwanzoni mwa mwezi huu kwa kile kinacho daiwa kuwa maeneo hayo ni sehemu ya hifadhi ya msitu wa Msaginya.

Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mgolokani wakiwa na familia zao chini ya mti ambapo sasa pamegeuzwa kuwa makazi.
Operesheni ya kuwaondoa wananchi katika maeneo mbali mbali mkoani Katavi inayofanywa kwa amri za wakuu wa wilaya imewaacha mamia ya wananchi bila makazi, huku maeneo mengine familia zikiathiriwa zaidi na maradhi.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...