MOGADISHU.
Jeshi la Marekani limesema kuwa limewaua wanachama sita wa kundi la
wanamgambo wa al-Shabab kwenye mashambulizi matatu ya angani kusini mwa
Somalia.
Kituo cha jeshi la
Marekani barani Afrika kimesema kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Somalia, jeshi
la Marekani limeendesha mashambulizi matatu ya angani nchini Somalia dhidi ya
kundi la al-Shabab ambapo wanamgambo 6 wameuawa.
Al-Shabab wametangaza
kutii kundi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira salama kwa mashambulizi ya
kigaidi kote duniani.
Pia wametangaza wazi
kujitolea katika kupanga na kuendesha mashambulizi dhidi ya Marekani na
washirika wake eneo hilo.
Jeshi la Marekani
linasema kuwa liitaendelea kutumia kila mbinu kuwalinda raia wake kutokana na
vitisho kutoka kwa magaidi kwa lengo na kuwashambulia magaidi na kambi zao za
mafunzo kote nchini Somalia na kote duniani.
@habari na Bbc swahili
No comments:
Post a Comment