Thursday, 14 September 2017

Rukwa: Askali ameuawa na watu sita kwa kipigo.



Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP Geroge Kyando



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwanarusi(32) mkazi wa kijiji cha Ilemba Mkoani Rukwa,ameuawa na watu sita baada ya kupigwa mateke na ngumi sehemu za ubavu wa kulia na kushoto.
Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP Geroge Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tukio hilo limetokea juzi majira ya usiku.
Kamanda Kyando amesema chanzo cha mauaji ni ugomvi wa kifamilia wakimtuhumu marehemu kwa kosa kutofika  kwenye msiba wa kaka yake aliyefariki Septemba 2 mwaka huu.

Kwa mjibu wa Kamanda Kyando,wauaji walimvizia kilabuni na kumkamata na kisha kuanza kumshambulia hadi kufa ambapo hata hivyo mtuhumiwa mmoja amekamatwa na anatarjiwa kufikishwa mahakamani huku juhudi za kuwatafuta waliokimbia zinaendelea.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...