Friday, 15 September 2017

(ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa





DAR ES SALAAM
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

ACP Mwakalukwa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu suala zima la uhalifu wa makosa ya mitandao ambapo kwa sasa limeshika kasi kubwa.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Thadayo Ringo amesema analishukuru jeshi la polisi kwa kuweza kuwasaidia katika kuwatatulia changamoto mbalimbali hasa za kiusalama huku akiwataka wananchi watakaopata matatizo katika mtandao kwenda kutoa taarifa polisi ili waweze kuwasaidia kabla ya kufika kwao.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...