Friday, 15 September 2017

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.


MPANDA

SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi,limesema watu wenye ulemavu mkoani Katavi bado wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo Mkoani Katavi Bw.Issack Lucas Mlela amesema,makundi ya watu wenye ulemavu yameendelea kuishi katika maisha magumu kutokana na kutopewa kipaumbele kama sheria ya nchi inavyoelekeza.

Aidha Bw. Mlela ameyapongeza mashiriki binafsi ambayo yamekuwa yakitoa semina kwa watu wenye ulemavu ili kutambua haki yao na wajibu wa jamii kuhusu makundi hayo.
Makundi ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi yanahusisha walemavu wasioona,walemavu wa viungo,viziwi,walemavu wa akili,walemavu wenye tatizo la usonji na wenye ulemavu wa ngozi Albino.


Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010 ,serikali pamoja na jamii kwa ujumla inawajibika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa na wale wasio na ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Uchumi, Biashara na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya binadamu.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...