Wednesday, 20 September 2017

Tetemeko laua zaidi ya watu 200 Mexico

Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusiHaki miliki ya pich
Image captionWaokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi
Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.
Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.
Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
Tetemeko laua zaidi ya watu 100, MexicoHaki miliki ya picha
Image captionTetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico
Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea.
''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sekunde thelathini tu, lakini ilionekana kama limedumu daima...'' anasema Daniel Lieberson.
Kwa upande wake Natasha Pizzey mwandishi wa habari katika mji huo anasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.
Juhudi za uokoaji zikiendeleaHaki miliki ya picha
Image captionJuhudi za uokoaji zikiendelea
''..Tunafahamu kuna watu walionusurika katika majengo ya makazi yaliyoporomoka, hatukuwa na uwezo wa kuwaokoa. Kuna mamia ya wafanyakazi wa kujitolea waliokwenda katika eneo la tukio...'' ameongezea kusema
Aidha pia kumetokea madhara mabaya katika majimbo ya jirani ya Morelos na Puebla.
Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
Tetemeko laua zaidi ya watu 100, Mexico
Image caption@habari toka Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...