KATAVI.
Jeshi
la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi limewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani hapa kufukia mashimo yote
yaliyowazi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani
Katavi Izrael Butika Ili kuepukana na majanga ya ufukiwaji na vifusi pamoja na
maporomoko yanayoweza kutokea kutokana na maji ya mvua katika kipindi hiki.
Ameongeza
kuwa katika kipindi hiki cha Mvua ni vizuri kwa wachimbaji hao wa
madini kutawanya vifusi vyote sambamba na kutoziba njia rasmi za maji katika
maeneo yao na kuhakikisha mashimo wanayochimba wanayawekea matimba.
Aidha
amewashauri wamiliki wa migodi kuwawekea mazingira mazuri na kuwasimamia
wachimbaji wadogo kufuata sheria za usalama mahali pakazi.
No comments:
Post a Comment