MPANDA
WAKAZI wa Mitaa ya Msasani na
Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameeleza kutoridhishwa na
mwenendo wa ugawaji viwanja katika mtaa wa kampuni kata ya Misunkumilo
wanakotakiwa kuhamia.
Wakizungumza na Mpanda Radio
wamesema,wamesikitishwa na kauli ya Mstahiki Meya Manispaa ya Mpanda William
Mbogo kwamba wanaotakiwa kupewa viwanja kwa sasa ni wazee, wajane na wasiojiweza huku wengine wakiachwa bila
kujua hatima yao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda
William Mbogo amekanusha eneo la kampuni kupewa wazee,wajane na wagonjwa peke
yao ambapo amesema mgao huo utafanyika kwa wahanga wote isipokuwa kipaumbele
kimetolewa kwa wasiokuwa na uwezo wakiwemo wazee.
Wakazi zaidi ya 200 za mitaa ya
Msasani na Tambukareli zinatakiwa kuondoka ndani ya mipaka ya hifadhi ya reli
kabla ya mwezi jaunuari mwakani.
No comments:
Post a Comment