Baada ya wawakilishi wa CDU na CSU kuzungumza na waliberali wa FDP, jioni ikawa zamu ya kukutana na wale wa walinzi wa mazingira die Grüne.
Pande zote nne zinaonyesha kuridhika na jinsi mazungumzo hayo yalivyoendelea, kama anavyosema katibu mkuu wa chama cha kansela Angela Merkel Christian Democratic Union CDU, Peter Tauber : "Ikiwa vyama ambavyo misimamo yao ni tofauti-na hilo limebainika katika mazungumzo-vinajaribu kushirikiana, basi hiyo ni ishara muhimu na hasa linapohusika suala la kuondowa kile kinacholeta mtengano katika jamii.
Tunabidi hata kusema baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo, njia ni ndefu hadi tutakapofikia msimamo wa pamoja. Na ndio maana tunasubiri kwa shauku kubwa duru ya kwanza ya mazungumzo ya pande nne, ijumaa inayokuja."
Kansela
Angela Merkel (kushoto) na mkuu wa kundi la wabunge wa walinzi wa
mazingira Katrin Göring-Eckerdt (kati) na mwenyekiti wa chamam hicho Cem
Özdemir (kulia)
Sifa zimetolewa pia na walinzi wa mazingira die Grüne na wahafidhina wa CSUNa mkuu wa shughuli za chama cha walinzi wa mazingira Michael Kellner amesifu pia mazungumzo hayo akisema wamezungumzia mada na ufumbuzi. Sawa na Tauber na yeye pia amesema njia bado ni ndefu hadi muungano wa vyama vinne unaojitambulisha na rangi nyeusi kwa vyama ndugu vya CDU/CSU, manjano kwa chama cha FDP na kijani kwa walinzi wa mazingira die Grüne, muungano wa Jamaica kama unavyoitwa, utakapoundwa.
Na katibu mkuu wa chama cha CSU, Andreas Scheuer amekiri aliposema kampeni za uchaguzi zimeshamalizika, mazungumzo yalikuwa muhimu na hali ilikuwa ya kuridhisha, hata hivyo anaongeza kusema mada muhimu zinabidi kujadiliwa.
Nembo
ya mazungumzo ya muungano unaoitwa wa Jamaica kati ya CDU/CSU(nyeusi),
FDP (Manjano) na walinzi wa mazingira die Grüne wanaojitambulisha na
rangi ya kijani.
Mazungumzo huenda yakadumu wiki kama si mieziMada hizo ni pamoja na suala la wakimbizi na kinga ya ukimbizi, sawa na nishati na sera kuelekea mabadiliko ya tabia nchi. Hii leo wawakilishi wa chama cha kiliberali cha FDP wanakutana na walinzi wa mazingira die Grüne.
Na ijumaa ndipo duru ya kwanza itakayowakutanisha wawakilishi wa pande zote nne itakapoitishwa mjini Berlin. Kwakua misimamo ya pande hizo nne inatofautiana mno, wadadisi wanakadiria mazungumzo hayo yatadumu muda mrefu kupita kiasi.
Binafsi kansela Angela Merkel anakadiria wiki kadhaa zitahitajika.
Kuna wanaokadiria mazungumzo yanaweza kuendelea hadi mwakani.
No comments:
Post a Comment