MPANDA
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wameeleza kuwa endapo sera ya
viwanda ikitekelezwa kwa vitendo itapunguza Wimbi la ukosefu wa ajira.
Kauli hiyo inajiri ikiwa ni siku chache baada
ya kuzinduliwa kwa sera ya Tanzania mpya ya viwanda iliyofanyika mkoani Dodoma iliyokwenda
samba mba na tamko la serikali kuwa kila mkoa uwe umejenga viwanda 100
Aida wameongeza kwa
kusema kuwa ni vema watu wote kujishughulisha ili kuweza kufikia uchumi wa
viwanda sanjari na kusaidia watu wengi ambao walikosa ajira na kuwepo mitaani kupata
fursa ya kuweza kujishughulisha.
Waziri Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
serikali za mitaa(Tamisemi) Seleman Jafo
alitoa tamko kwa wakuu wa mikoa wote kuwa
disemba mwaka huu hadi mwakani mikoa yote 26 ya Tanzania bara inapaswa
kujenga viwanda 100.
No comments:
Post a Comment