Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Michael Nzungu |
MPANDA
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani katavi Michael Nzungu amesema
wamedhamiria kununua gari kwa ajili ya uzoaji taka wanachosubiri ni kibali
kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu.
Akizungumza na mpanda
redio amesema kwa sasa wanakodi gari ambalo bado halikidhi mahitaji ya mkoa
hivyo wameanza kujihada za kununua gari
ambalo mwaka huu litakuwa limeanza kazi.
Aidha amesema wananchi
wawe wavumilivu katika kipindi kifupi kilichobaki ili waweze kutatua kero ya
kuzagaa kwa taka kwani gari dogo la manispaa linalotumika kwa sasa halitoshi
kubeba taka zote .
Amewataka wananchi
kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapoona taka zimerundikana ili
utaratibu wa kuziondoa uweze kufanyika.
No comments:
Post a Comment