Wednesday, 15 November 2017

Serikali itazidisha juhudi katika kulisimamia zao la mwani ili liweze kutoa tija kwa wakulima wazao hilo.



Wakulima wa mwani zanzibar


ZANZIBAR

Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema  serikali itazidisha juhudi katika kulisimamia zao la mwani ili liweze kutoa tija  kwa wakulima wazao hilo.

 Akizungumza na vyombo vya  kufuatia malalamiko ya wakulima  kuwa na  bei ndogo ya zao hilo    amesema  kwasasa bei ya mwani inashuka  kutokana na  kuuzwa nje ya nchi lakini  ili kuwarahisishia  wakulima  watawapatia  mashine za kusagia  mwani ambazo  zitasaidia  kuondokana na  tatizo hilo.

 Amesema kwa  sasa wameshaweka mashine  mbili kwa upande  wa unguja na mbili wanatarajia  kupeleka  pemba  ili kurahisisha  upatikanaji wa unga  wa mwani  ambao   unauzwa  kwa bei ghali.

 Aidha amewataka wakulima  kuongeza jitihada  juu ya kilimo hicho  kwani serikali inaendeleza juhudi  za kuhakikisha  zao hilo  linawanufaisha  wakulima  kutokana na umuhimu wake  katika matumizi mbalimbali ya  binadamu.

Source: mwananchi 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...