Wednesday, 15 November 2017

Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali maombi ya muungano wa upinzani NASA ya kushirikishwa kwenye madai ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

NAIROBI

 Maamuzi hayo ni pigo kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na muungano wa vyama vya kisiasa anaouongoza wa NASA.

 Mwanasheria na wanaharakati wawili wa kutetea haki za binadamu waliwasilisha madai dhidi ya ushindi wa Rais Kenyatta wakidai kwamba uchaguzi ulikuwa batili kwa sababu uteuzi mpya wa wagombeaji haukufanyika.

Maamuzi hayo maana yake kwamba Kenyatta anaweza kuapishwa tarehe 28 mwezi huu wa Novemba ikiwa matokeo ya uchaguzi yatathibitishwa.

Source: Dw swahil

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...