Wednesday, 15 November 2017

Shirika la kazi duniani ILO yalenga kuangamiza ajira ya watoto.




Kongo Kobalt-Abbau (picture alliance/AP Photo/S. van Zuydam)
Shirika la kazi duniani  ILO limetoa wito wa kuimarishwa juhudi za kuangamiza ajira ya watoto ndani ya miaka minane.
Mmoja kati ya watoto 10 kote duniani ni waathiriwa wa ajira ya watoto, na karibu nusu yao wanafanya kazi hatari. Hayo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani Guy Ryder.
Ryder amekiri kwamba idadi ya wafanyakazi watoto imepungua kwa milioni 100 tangu mwishoni mwa miaka ya 90, wakati alipozungumza kwenye ufunguzi kongamano la kimataifa kuhusu suala hilo mjini Buenos Aires. Lakini alilalamika kuwa kiwango cha mabadiliko kimepungua sana katika siku za karibuni.
Türkei | Syrische Flüchtlingskinder arbeiten in einer Textilfabrik in Gaziantep (Getty Images/C. McGrath)
Mtoto mkimbizi wa Kisyria akishona viatu Uturuki
"hatuwezi kubashiri jinsi masoko ya ajira yatabadilika katika siku za usoni, lakini tunafahamu kitu kimoja: hatutaki tena ajira ya watoo na utumwa mamboleo”, alisema Ryder.
Kwa mujibu wa makadirio ya ILO, kuna wafanyakazi watoto milioni 152  na waathiriwa milioni 25 wa ajira ya kulazmishwa kote duniani.
Kongamano hilo, la nne na la aina yake, lilisisitiza kuhusu lengo lake la kumaliza ajira ya kazi ifikapo mwaka wa 2025.
Afrika yaangaziwa
Wito wa Ryder umekuja wakati Shirika la kimataifa la haki za binadamu- Amnesty International likielezea jinsi karibu nusu ya makampuni 28 makubwa duniani bado yanatumia madini ya cobalt ambayo yalichimbwa na wafanyakazi watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kutumiwa kutengeneza betri.
Katika ripoti yake, yenye kichwa Time to Rechearge, kundi hilo la kutetea haki za binaadamu limeyataja makampuni ya Microsoft, Renault na Huawei ya China kuwa miongoni mwa wanaonufaika na ajira ya watoto.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa hakuna kampuni yoyote kati ya hayo 29 yaliyochungzwa, iliyotimiza majukumu yake ya kufichua na kupunguza matukio ya ukiukaji wa haki za binaadamu. Sekta ya kutengeneza magari nchini Ujerumani pia ina hatia, kwa mujibu wa ripoti hiyo. wakati kampuni ya BMW inafanya vyema katika mambo kadhaa” na kuyashinda makampuni mengine, inaendelea kuonyesha mapungufu makubwa. Amnesty pia imesema makampuni ya Volkswagen na Daimler pia wana mapungufu makubwa.Amnesty inasema watoto wa hadi chini ya umri wa miaka saba wanahatarisha maisha yao na afya yao kutimiza mahitaji ya madini ya Cobalt, kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya betri kwenye magari ya umeme, simu za smartphone na nishati jadidifu.
Madai hayo pia yametolewa kwa makampuni mengine makubwa ya vifaa vya elektroniki, ikiwemo Apple, Samsung na Sony, ambayo yanaendelea kunufaika na ajira ya watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...