MPANDA
Wanaharakati wa kutetea haki za watu
wenye ulemavu wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kusimamia kanuni
na sheria za nchi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu kama zilivyoainishwa
katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Wanaharakati hao wakiwemo mtandao wa
wazazi,Shivyawata, wajumbe wa baraza la watoto wilayani Mpanda na kamati ya
kulea baraza la watoto,wametoa kauli hiyo leo katika kikao cha kujadili haki za
watoto wenye ulemavu kikao ambacho kimefanyika mjini Mpanda.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa
Elimu Jumuishio Mkoani Katavi Bw.Raphael Fortunatus Jumbe pamoja na kueleza lengo la
semina y aleo anabainisha makundi ambayo yameshirikishwa.
Kwa mjibu wa vifungu vya sheria ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawaziri katika wizara husika
wanatakiwa kusimamia misingi yote inayompa haki za msingi mtu mwenye ulemavu
anapohitaji kuhudumiwa bila ubaguzi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi SHIVYAWATA Bw.Issack
Lucas Mlela ambaye pia ni mjumbe wa katamati ya kulea baraza la watoto wenye
ulemavu pamoja na mambo mengine amesema sheria namba 9 ya mwaka 2010 inasimamia
haki za watu wenye ulemavu huku akisema wakati mwingine unyanyapaa nao unaanzia
kwa ndugu wenyewe kumnyanyapaa mwenye ulemavu suala ambalo halitakiwi
likubalike.
Baadhi ya ibara zilizopo katika
katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ambazo zinatakiwa zisimamiwe vizuri
ili watu wenye ulemavu wapate haki zao ni pamoja na ibara ya
4,20,26,27,28,31,32 na 34 ambavyo vinaitaka serikali ya Tanzania kutekeleza
haki zote za msingi kwa watu wenye ulemavu katika Nyanja mbalimbali ikiwemo
sekta ya afya,elimu,ajira na haki nyingine za kibinadamu.
Licha ya ibara hizo pia Tanzania ni
miongoni mwa nchi za jumuiya ya madola ambazo zilisaini mikataba mbalimbali kwa
ajili ya kusimamia na kutekeleza haki za watu wenye ulemavu.
Katika kipindi cha mwaka 2014 mpaka 2016
jumla ya watu wenye ulemavu 83 wakiwemo watoto wenye umri wa kwenda shule
wametetewa na mradi wa elimu jumuishi wilayani Mpanda na kupatiwa haki zao
muhimu kama elimu.
source. Isack Gerald
No comments:
Post a Comment