Unguja.
Watendaji
na viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kufuata falsafa za ‘hapa
kazi tu na kutofanya kazi kwa mazoea ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora
kwa wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaim Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud
wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama, watendaji
wa serikali za halmashauri za wilaya na Mkoa huo katika mkutano wa tathmini
uliofanyika kwenye ukumbi wa vyuo vya amali Mkokotoni.
Ayoub amesema
katika ziara yake ya siku 5 aliyoifanya katika mkoa huo, amegundua
kuwepo kwa kasoro na mapungufu ya kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hizo na
kusababisha wananchi wengi kutokuwa na imani na serikali yao kwa kukosa huduma
muhimu za kijamii
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi wa Wilaya na Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Hassan
Ali Kombo amesema wakati umefika kwa viongozi kutekeleza majukumu yao kwa
wakati hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuondoa malalamiko
kwa wananchi.
Pia mkuu
wa wilaya huyo ameahidi kuyanyia kazi kwa wakati maagizo na miongozo
iliyotolewa na kaimu mkuu wa mkoa ili kupunguza matatizo yanayowakabili
wananchi wa Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment