Thursday, 2 November 2017

Wananchi wa Kata ya katumba katika halmashauri ya Nsimbo wametakiwa kudumisha amani, upendo na mshikamano baina yao.


MPANDA.

Wananchi wa Kata ya katumba katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wametakiwa kudumisha amani,  upendo na mshikamano baina yao.

Wito huo umetolewa na diwani wa kata Ya katumba Seneta Baraka wakati akizungumza na Mpanda redio hapo jana.

Amesema kuwa wananchi hawana budi kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii ili kuweza kuleta maendeleo.

Katika hatua nyingine amewataka wahudumu wa Afya katika kata yake kufanya kazi kwa maadili yao ikiwa pamoja na kuacha kuwanyanyasa wananchi wanaokwenda kupata huduma.


@habari na mwandishi wetu ALINANUSWE EDWARD

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...