Saturday, 16 December 2017

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi Mkoani Katavi.



Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon

 

KATAVI 

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi Mkoani Katavi.
Katika taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Kwayi,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni saba zimekwishatumika katika ujenzi wa zahanati hiyo huku akisema zinahitajika fedha nyingine zaidi ya milioni ishirini na tisa ili jingo likamilike na kuanza kutoa huduma mwakani 2018.
Kwa upande wake IGP sirro mara baada ya kupokea taarifa hiyo amesema jeshi la polisi litaongeza takribani milioni kumi na Tano ili kuunga juhudi za ujenzi wa zahanati hiyo.
Wakati huo huo IGP siro amesema unahitajika mkakati wa haraka ili kujenga nyumba za polisi ili kuondoa uhaba uliopo kwa sasa na kuagiza mkoa uanze kufanya mikakati wa haraka.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa dini mkoani Rukwa,Kuongeza bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo na imani za kishirikina na wivu wa kimapenzi yapungue mkoani humo.





Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon     
 RUKWA
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa dini mkoani Rukwa,Kuongeza bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo na imani za kishirikina na wivu wa kimapenzi yapungue mkoani humo. 

IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na mauaji mkoani humo.

Amesema jeshi la polisi linajitahidi kukabiliana na mauaji yote yanayotokea nchini lakini katika Mkoa wa Rukwa takwimu zinaonesha kuwa mauaji yanayotokana na ushirikina pamoja na  wivu wa mapenzi yanaongoza mkoani humo.

Wakati huo huo IGP Sirro ameahidi kuwa Jeshi hilo kupitia bajeti zake litajenga kituo kipya cha polisi cha Sumbawanga mjini ambacho ni chakavu kwa sasa huku akiahidi pia kuupatia mkoa wa Rukwa gari moja jipya aina ya Lori litakalosaidia kutumika katika matumizi mbalimbali ya polisi mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya wa ulinzi na usalama mkoani Rukwa Joachim Wangabo ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo amemwambia IGP kuwa atajitahidi kuwashirikisha wafanyabiashara mkoani humo ili wajenge nyumba za kuishi polisi kwa kuwa hawawezi kusubiri mpaka serikali ifanye kazi hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema ushauri wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka kuongezwa muda wa urais kutoka miaka mitano mpaka miaka saba ni suala zuri na linazungumzika bila matatizo.


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd

ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema ushauri wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka kuongezwa muda wa urais kutoka miaka mitano mpaka miaka saba ni suala zuri na linazungumzika bila matatizo.

Balozi Idd amebainisha hatua hiyo wakati akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Tisa la Wawakilishi lililochukua muda wa wiki moja Mjini Zanzibar.

Awali baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 1984 na kuweka sheria ya mwaka 2017 wamesema ili Zanzibar iepukane na matumizi hasa kipindi cha uchaguzi hakuna budi kuongezwa kwa muda wa utumishi wa urais.

Hata hivyo,Balozi Iddi akifunga mkutano huo amesema Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake ili kuona nao wanaishi katika hali ya matumiani.

Ikulu ya Marekani imesema inapanga kuanzisha upya juhudi za kufikiwa makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina licha ya uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.





WASHINGTON DC
Ikulu ya Marekani imesema inapanga kuanzisha upya juhudi za kufikiwa makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestina licha ya uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Maafisa wa utawala wa Marekani wamesema juhudi hizo huenda zikafufuliwa wiki ijayo kukiwa na matumaini kuwa ghadhabu dhidi ya hatua aliyoichukua Trump itakuwa imepungua.

Rais Mahamoud Abbas wa Palestina alitangaza mapema wiki hii kuwa Wapalestina hawatakubali Marekani kuwa na jukumu lolote katika mchakato wa kutafuta amani katika mzozo wa Mashariki ya Kati kwa sababu Marekani inaipendelea Israel.

Kufuatia hatua hiyo,viongozi wa Palestina walisema hawatakutana na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence anayetarajiwa kuwasili mjini Jerusalem Jumatano ijayo kwa ziara Mashariki ya Kati. 

Ikulu ya Marekani imesema inatumai ziara ya Pence itakuwa sehemu ya kile ilichokitaja kama kufungwa kwa ukurasa mmoja na kufunguliwa mwingine wakiendelea kuangazia kufikiwa kwa amani Mashariki ya Kati.
Chanzo:Dw swahil

Chama tawala cha ANC nchini Afrika kusini kinafanya mkutano mkuu kumteua kiongozi mpya wa chama hicho.



Wagombea wakuu ni Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril Ramaphosa


JOHANESBURG
Chama tawala cha ANC nchini Afrika kusini kinafanya mkutano mkuu kumteua kiongozi mpya wa chama hicho.
Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.
Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.
Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.
Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg.
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini anatarajiwa kuhutubia wajumbe wanaohudhuria mkutano huo mkuu.

Wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.
Kivumbi hasa kipo katika Kinyanganyiro cha kumrithi rais Zuma, kama kiongozi wa chama ni kati ya mkewe wa zamani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma  ambae pia aliwahi kuwa waziri na vilevile alikuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika.

Lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa,
Mvutano huu pamoja na kashfa chungu nzima hasa za rushwa zinazomuandama rais Jacob Zuma zimeongoza hofu za kugawanyika kwa ANC.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili.
Chanzo:Bbc swahil


Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...