Thursday, 7 December 2017

Mauaji Kibiti, chanzo cha Mwandishi kupotea?


Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wanaamini kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi kwa siku 17 sasa ni kwa nia mbaya.

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Teofile Makunga anasema kama mwandishi huyu angekuwa anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa sababu yoyote angetakiwa kuwa amefikishwa mahakamani kufikia sasa.

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai ameomba vyombo vya ulinzi na usalama kuzidisha kasi ya kumtafuta mwanahabari huyo ambaye ametoweka kwa zaidi ya siku kumi sasa.

Wahariri wanapanga kufanya maandamano ya kushinikiza kuzidishwa kazi kwa msako huo yatakayoanzia mnazi mmoja hadi makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam.

Bwana Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauwaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo.

Source Eatv

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...