Wednesday, 13 December 2017

NEC yamvimbia Mbowe.


DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, Ramadhan Kailima, amesema, chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume ihairishe kwa kuwa haiko kumshawishi mtu au chama kushiriki.
Kailima amesema, chama kushiriki uchaguzi ni jambo la hiari na NEC ipo kwa ajili ya kuweka na kutengeza mazingira yatakayofanya vyama vya siasa kushiriki uchaguzi na iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi, kitakachoshiriki hata kama ni kimoja mgombea wake atapita bila kupingwa.
Aidha, Kailima ameviasa vyama vya siasa vinavyotishia kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na kata sita Januari 13,2018 kufuata mifumo ya kisheria ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi.
Mapema wiki hii muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi, (UKAWA), kupitia kwa mmoja wa Wenyeviti wake, Freeman Mbowe, alitishia kuwa umoja huo hautoshiriki uchaguzi iwapo changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 Novemba 26, hazitafanyiwa kazi na NEC.

Chanzo: EATV

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...