Thursday, 7 December 2017

Umoja wa Ulaya unatarajia kufungua mashitaka dhidi ya Poland, Hungary na Jamhuri ya Czech kwa hatua yao ya kukataa kuwapokea wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya kisiasa.

JENEVA

Umoja wa Ulaya unatarajia kufungua mashitaka dhidi ya Poland, Hungary na Jamhuri ya Czech kwa hatua yao ya kukataa kuwapokea wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya kisiasa.

 Hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa vyanzo viwili vya habari kutoka Umoja wa Ulaya.

 Umoja wa Ulaya umesema nchi hizo tatu zimeshindwa kuonyesha mshikamano na nchi washirika ambazo zimekubali kuwapokea wahamiaji.

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Czech Milos Zeman hapo jana Jumatano amemteua mfanyabiashara bilionea Andrej Babis kuwa waziri mkuu.

Chama cha Babis kiitwacho -ANO kilishika nafasi ya kwanza katika uchaguzi wa Oktoba baada ya kuahidi kuzuia uhamiaji.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...